Kiongozi wa upinzani nchini uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ametangaza kurejea nyumbani baada ya kutorokea uhamishoni.
Kyagulanyi wa chama cha National Unity Platform (NUP) alikimbia nchini Uganda akipitia Rwanda na kusafiri hadi Marekani, baada ya uchaguzi mkuu wa Januari 15 mwaka huu.
Wine alitoroka Uganda kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Urais ambapo alizoa kura milioni 2.7, ikiwa asilimia 24 ya kura zote dhidi ya Rais Yoweri Museveni aliyepata kura milioni 7.9.
Akiwa Marekani Kyagulanyi amefanya mikutano kadhaa na Waganda wanaoishi Marekani.