Rais William Ruto wa Kenya siku ya Jumatatu amekutana na mwenyeji wake Rais Sergio Mattarella wa Italia mjini Rome.
Ruto amewasili Italia mapema leo kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu.
Awali Rais aliweka shada la maua katika kaburi la wanajeshi waliouawa la Piazza mjini Venezia.

Akiwa Italia Ruto anatarajiwa kusaini mikataba kadhaa ya ushirikiano baina ya Kenya na Italia.