Matayarisho yakamilika kwa Kip Keino Classic

Kwa mara ya kwanza teknolojia ya kuwasaidia wanariadha kuongeza  kasi maarufu kama Wavelight itatumika humu nchini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Matayarisho yamekamilika kwa makala ya saba ya mashindano ya Kip Keino Classic continental Tour, yatakayoandaliwa Ijumaa hii katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Kwa mara ya kwanza teknolojia ya kuwasaidia wanariadha kuongeza  kasi maarufu kama Wavelight itatumika humu nchini.

Mkurugenzi wa mashindano hayo ya nembo ya dhahabu Barnaba Korir ,akiwahutubia wanahabari Jumatatu jijini Nairobi, amesema watashirikisha pia mashindano ya watoto ambayo yatafungua pazia.

“Mashindano ya mwaka huu yanaashiria azma yetu ya kuandaa mashindano ya hadhi ya kimataifa,na tayari tuko na majina tajika kutoka humu nchini na kimataifa ,tutawashirikisha watoto katika mashindano ya Ijumaa kwa mara ya kwanza.”akasema Korir

Bingwa wa Olimpiki katika mita 200 Garby Thomas wa Marekani atatimka mbio za mita 100 wanawake huku pia bingwa wa Jumuia ya madola Ferdinand Omanyala akikabiliana na Mark Otieno katika mita 100.

Mashindano yataandaliwa kati ya sa kumi hadi saa mbili usiku na yatakuwa ya mzunguko wa pili duniani baada ya yale ya Australia mwezi jana.

 

 

Share This Article