Waziri Duale azindua maafisa wapya wa Baraza la KMPDC

Akizungumza baada ya kuzindua baraza hilo Duale, ametaja wajibu muhimu unaotekelezwa na wataalam hao katika afya ya jamii  na kusisitiza haja ya kuzingatia kanuni za kitaaluma.

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Afya nchini Kenya  Aden Duale siku ya Jumatatu amezindua Baraza jipya la matabibu na wataalam wa meno  nchini (KMPDC) , itakayoongozwa na Profesa  Namenya Were.
Akizungumza baada ya kuzindua baraza hilo Duale, ametaja wajibu muhimu unaotekelezwa na wataalam hao katika afya ya jamii  na kusisitiza haja ya kuzingatia kanuni za kitaaluma.
Waziri pia alitaja mabadiliko yanayoendelea katika sekta  hiyo yatakayopiga jeki juhudi za serikali za kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.
Alilitaka baraza hilo kuwa katika mstari wa mbele kuleta mabadiliko mwafaka  ya kuleta uwazi na usimamizi bora.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Katibu wa Afya ya umma Mary Muthoni,Mkurugenzi mkuu wa Afya Dkt Patrick Amoth,na Afisa Mkuu mtendaji wa KMPDC David Kariuki miongoni mwa viongozi wengine wa wizara ya afya.
Share This Article