Lokedi na Korir wawinda ushindi wa pili Boston Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha wa Kenya Sharon Lokedi na John Korir ,watajitosa katika barabara za mjini Boston Marekani Jumatatu jioni wakilenga kuhifadhi  mataji ya mwaka jana ya Boston Marathon.

Lokedi aliyeshinda mbio za mwaka jana akiweka rekodi mpya ya  saa 2 dakika 17 na sekunde 22 ,  atawaongoza Wakenya wenza  wakiwemo Irene Cheptai,Loice Chemnung ,Mary Ngugi Cooper,na Mary Chelangat.

Wakenya hao watapata upinzani mkali kutoka kwa Waethiopia kama vile;Workenesh Edesa, Bedatu Hirpa  na  Fikirte Woleta.

Bingwa wa  kilomita 10 wanaume katika mashindano ya Sirikwa classic John Korir anayejivunia muda bora kwa wanaume wa saa 2 dakika 2:24, pia atatetea taji yake.

Aidha,  mashidano hayo ambayo ni ya pili katika msururu wa mbio kuu za marathon baada ya Tokyo Marathon mwezi uliopita zitawashirikisa pia Wakenya wengine Benson Kipruto, Cybrian Kotut, Alex Masai, Bernard Biwott na  Kennedy Kimutai.

 

 

Share This Article