Wenyeji Morocco ndio timu ya kwanza kujikatia tiketi kwa robo fainali ya makala ya 14 ya kipute cha Kombe la mataifa ya Africa-WAFCON,kufuatia ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya majirani Algeria,Alhamisi usiku uwanjani Prince Moulay Hassan jijini Rabat.
Kipindi cha kwanza kilimalizikia sare tasa na mechi ikielekea ukingoni wenyeji walipata bao kupitia kwa
Sanaa Mssoudy aliyeunganisha krosi ya Hanane Ait El Haj kufuatia uzembe wa walinzi wa ALgeria.
The Atlas Lionesses watacheza mechi ya mwisho Agosti 3,dhidi ya Senegal ambayo imefufua matumaini ya kuingia nane bora baada ya kuwalemea Kenya pia goli moja kwa nunge.
Kenya iliyaaga mashindano baada ya kupoteza mechi mbili mtawalia.