Serikali imetangaza mfumo mpya wa kuwatuza wanamichezo chipukizi watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kuanzia kwa mashindano ya riadha Duniani kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20, yatakayoandaliwa mjini Eugene,Oregon,Marekani kati ya tarehe 5 na 9 mwezi ujao.
Waziri wa michezo Salim Mvurya akikabidhi benderea ya taifa kwa timu hiyo jana, ametangaza kuwa washindi wa dhahabu watatuzwa shilingi milioni 2,nishani ya fedha milioni 1.5 na shilingi milioni 1 kwa watakaoshinda medali za shaba.
Aidha,Mvyurya amesema serikali inatayarisha mfumo mpya wa kuzituza timu za michezo nchini kama njia ya kuwamotisha wachezaji.
Kikosi cha Kenya kinachowajumuisha wanariadha 23, wakiwemo wavulana 12 na wasichana 11 kitaondoka nchini Jumamosi hii kuelekea marekani.
Kenya inalenga kuboresha matokeo ya mwaka 2024 mjini Lima, Peru, ilikomaliza ya tano kwa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 1.