Timu ya taifa ya Jamhuri ya Demokrasia (DRC) imelazimika kuhamishia kambi ya fainali za Kombe la Dunia nchini Ubelgiji kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola mjini Kinshasa.
Hali ya ugonjwa wa Ebola imekuwa mbaya nchini DRC huku watu 139 wakiuawa na visa 600 kunakiliwa.
Shirika la Afya Duniani (WHO ) limetangaza ugonjwa wa Ebola kuwa dharura ya kiafya ingawa imesema sio janga.
Kufikia sasa, hakuna chanjo wala tiba kamili ya Ebola huku WHO ikisema huenda ikachukua hadi miezi tisa kabla ya kupatikana kwa chanjo yake.
Chui wa Congo wamefuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka huu tangu mwaka 1974.
DRC watafungua ratiba ya mazoezi Juni 3 kwa mchuano wa kirafiki dhidi ya Denmark mjini Liege na Chile, tarehe 9 mwezi ujao mjini Marbella.