Marekani imesitisha msaada mara moja kwa Afrika Kusini kufuatia agizo la Rais Donald Trump.
Katika agizo hilo,Trump alisema ameondoa msaada wote kupinga sera ya ubaguzi wa rangi wa serikali ya Afrika Kusini ya kuwatimua wazungu nchini humo na kutwaa mali yao.
Bilionea wa Marekani mzaliwa wa Afrika Kusini Ellon Musk, ambaye ni mshirika mkuu wa Trump, ameshutumu vikali sheria hizo za kiubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.