Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linasema kuwa linafuatilia taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii zinazodai kutekwa kwa David Joseph Jumbe, Msaidizi wa Mwenyekiti wa Kitaifa wa Chadema na watu wasiojulikana.
”Katika ufuatiliaji wa tukio hilo, polisi wanasema kuwa walifanikiwa kupata gari jeusi aina ya Toyota Wish alilokuwa ameabiri Jumba kabla ya kukamatwa na watu hao wasiojulikana,” ilisema katika taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita.
Hapo awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara Amani Golugwa alitoa taaria za kuthiibitisha kupatikana kwa David Jumbe akiwa na pingu mkononi.
Golugwa aliongeza kuwa maafisa wa Jeshi la Polisi walifika katika makao makao mkuu ya Chadema asubuhi ya leo Alhamisi na kusema kuwa wanamtafuta mtu anayedaiwa kutoroka akiwa na pingu.
”Walikuwa wanadai Jumbe amejificha ndani ya ofisi za Chadema na wanamtafuta ili wamfungue pingu,” alisema Golugwa aliyenukuliwa na Gazetui la Mwanachi.
Baadaye mke wa Jumbe alithibitisha kuwa mume wake amerejea nyumbani.
Taarifa ya BBC