Mabingwa wa Kombe la Dunia katika makala ya 23 yatakayoanza kesho Alhamisi, Juni 11 hadi Julai 19, watatuzwa shilingi bilioni 6.9 za Kenya, sawia na dola milioni 53.5 za Kimarekani.
Kiwango hiki ni ongezeko la kutoka kwa kima cha shilingi bilioni 5.4, walizotuzwa Argentina walipotwaa ubingwa mwaka 2022 nchini Qatar.
Timu ya pili itatuzwa shilingi bilioni 4.7, nambari 3 bilioni 4.2, huku timu ya nne ikiondoka na shilingi bilioni 3.9.
Timu zitakazomaliza katika nafasi za 9 hadi 32 zitapokea shilingi bilioni 1.8 kila moja, huku zile za kuanzia nafasi za 33 hadi 48 zikitia kibindoni shilingi bilioni 1.6 kila moja.
Kipute cha kombe la Dunia kinachoandaliwa nchini Mexico, Canada na Marekani, kitaanza rasmi kesho kwa pambano la ufunguzi kati ya Mexico na Afrika Kusini kundini A.
Jumla ya mechi 104 zitasakatwa katika viwanja 16 vilivyo katika miji 16 tofauti.