Matata wa Kenya ashinda Ras Al Khaimah half Marathon

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkenya Alex Matata ndiye bingwa wa makala ya mwaka huu ya mbio za Ras Al Khaimah Half Marathon zilizoandaliwa mapema leo katika Milki za Kiarabu./strong>

Matata ameziparakasa mbio hizo kwa dakika 59 na sekunde 20, akifuatwa na Mwethiopia Gemechu Dida kwa dakika 59 na sekunde 25, huku Mkenya mwingine Isaia Lasoi, akimaliza wa tatu sekunde moja baadaye.

Judy Kemboi wa Kenya amemaliza wa pili katika mbio za wanawake akizitimka kwa saa 1 dakika 6 na sekunde 34, akifuatwa na Jesca Chelangat kwa saa 1 dakika 6 na sekunde 53.

Ejgayehu Taye wa Ethiopia alishinda mbio hizo kwa saa 1 dakika 5 na sekunde 52.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *