Serikali ya kaunti ya Nairobi yawaajiri maafisa 35 wa sheria

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja.

Serikali ya kaunti ya Nairobi imewaajiri maafisa 35 wa sheria ili kupiga jeki utoaji huduma na kupunguza gharama ya kutafuta huduma za sheria kutoka nje.

Akizungumza Ijumaa wakati wa kufunga warsha ya siku mbili ya maafisa hao wa sheria, Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja alisema hatua ya kuwaajiri mawakili hao itasaidia pakubwa kulainisha matumizi ya shughuli za sheria katika kaunti hiyo.

“Tuna matarajio makubwa sana ya kufanikiaha manifesto yetu. Mboreshe maadili na msilete vizingiti kwa kushirikiana kusambaratisha shughuli za kaunti,” alisema Gavana Sakaja.

Gavana Sakaja alitoa wito kwa kundi hilo la mawakili kubuni mikakati thabiti ya kisheria.

“Hata mkikumbana na changamoto, msife moyo. Kumbukeni kuwa mnabadiliaha maisha na kurejesha Imani,” aliongeza Gavana huyo.

Sakaja aliwahakikishia mawakili hao kuwa atawaunga mkono mawakili hao wanapotekeleza majukumu yao.

Mkuu wa wafanyakazi wa kaunti hiyo David Njoroge, aliwataka maafisa hao wa sheria kutekeleza wajibu wao kwa bidii kwa wakazi na serikali ya kaunti ya Nairobi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *