Vifo vya Ebola vyazidi 2000 nchini DRC

Watu wengine 4,300 wamethibitishwa kuambukizwa.

Marion Bosire
1 Min Read

Takwimu za serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, zinaonyesha kwamba watu 2,011 wamefariki kutokana na mlipuko wa Ebola, huku wengine 4,300 wakithibitishwa kuambukizwa.

Mlipuko huo umetajwa kuwa miongoni mwa milipuko mikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo. Virusi vipya vya aina ya Bundibugyo vinaendelea kusababisha hofu kubwa.

Takribani wagonjwa 704 wamelazwa na kutengwa katika hospitali mbalimbali, ambapo maafisa wa afya wanaendelea na juhudi za kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Hata hivyo, utoaji wa misaada katika maeneo ya vijijini umeendelea kuwa changamoto, baadhi ya wahudumu wa afya wakigoma wakidai kutolipwa mishahara yao tangu mlipuko huo ulipotangazwa.

Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Mohamed Yakub Janabi, amesema kasi ya kuenea kwa virusi hivyo ni kubwa, na kuwaweka wahudumu wa afya katika changamoto kubwa ya kuvidhibiti.

Wakati huo huo, WHO imesema kwamba mlipuko huo ulidumu kwa muda kabla ya kugunduliwa rasmi.

Share This Article