Chama kipya cha kisiasa chazinduliwa Lamu

Chama hicho kiitwacho Chama Cha Ujenzi (CCU) na ambacho code yake ni 916 kimeahidi kupigania haki za jamii zilizotengwa nchini.

Martin Mwanje
1 Min Read
Umra Omar aliyekalia punda (kushoto) na ambaye ni mwasisi wa Chama cha Ujenzi

Idadi ya vyama vya kisiasa nchini iliendelea kuongezeka kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 baada ya kuzinduliwa kwa chama kipya katika kaunti ya Lamu leo Alhamisi. 

Chama hicho kiitwacho Chama Cha Ujenzi (CCU) na ambacho code yake ni 916 kimeahidi kupigania haki za jamii zilizotengwa nchini.

Kimezinduliwa na Umra Omar kutoka Lamu na kiko na alama ya punda ambaye ni mnyama aliyesemekana kutumika kwa ujenzi wa Lamu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chama hicho katika kisiwa cha Lamu, Omar ambaye alikuwa akiendesha punda, amesema CCU itajumuisha jamii zote nchini bila ubaguzi ili kujenga taifa zima.

Omar amesema kwa sasa, wanaanza kampeni ya kuhamasisha jamii zote nchini kuhusu chama hicho na kuandikisha wanachama.

Amedokeza kuwa kuwa wanapanga kuandikisha watu 50,000 kufikia mwisho wa wiki hii.

Share This Article