Bingwa mara mbili wa Olimpiki Eliud kipchoge ameibuka mshindi wa mbio za Melbourne nchini Australia mapema Jumapili ukiwa ushindi wa kwanza katika mbio za kilomita 42, baada ya miaka mitatu.
Kipchoge aliye na umri wa miaka 41 amesajili ushindi wake wa 17 kwa jumla katika marathon kwa muda wa saa 2 dakika 9 na sekunde 10.
Kipchoge alikuwa ameshinda marathon kwa mara ya mwisho mwaka 2023, alipotwaa ubingwa wa Berlin Marathon.
Thomas Do Canto na Reece Edwards wa Australia walimaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia.