Juniors Starlets waanza mazoezi mjini Casablanca kujiandaa Kombe la Dunia

Junior Starslets walitua Morocco mwishoni mwa wiki jana baada ya kambi ya mazoezi ya wiki moja nchini Uhispania.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 ,imeanza mazoezi yake mjini Casablanca -Morocco, kujiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia kuanzia Jumamosi hii.

Junior Starslets walitua Morocco mwishoni mwa wiki jana baada ya kambi ya mazoezi ya wiki moja nchini Uhispania.

Starlets wanaoishiriki Kombe la Dunia kwa  mara ya pili watafungua Kombe la dunia kundini E dhidi ya  Uchina Jumatatu ijayo Oktoba 19, kabla ya kumenyana na Marekani siku mbili baadaye.

Vipusa hao wanaofunzwa na Mildred Cheche watakamlisha ratiba ya kundi hilo dhidi ya Samoa Oktoba 25.

Fainali ya mashindano hayo yanayoandaliwa Morocco kwa mara ya pili mtawalia itasakatwa Novemba 7.

Share This Article