Rais William Ruto leo alirejelea ahadi yake ya awali ya punguza mzigo wa ushuru kwa wafanyakazi wa kipato cha chini.
Alisema kwamba serikali inapanga kuwaondolea ushuru wa PAYE wanaopata mshahara wa shilingi 32,333 na chini kwa kila mwezi.
Akiwahutubia Wakenya wakati wa Hotuba ya Hali ya Taifa Bungeni leo Novemba 18, 2026, Ruto alisema hatua hiyo inalenga kuongeza mapato ya wafanyakazi na kupunguza gharama ya maisha.
Rais pia alipendekeza kuondolewa kwa ushuru wa stempu kwenye miamala ya ardhi yenye thamani ya shilingi milioni 1 au chini.
Aidha, serikali inapanga kuondoa ushuru wa asilimia 25 unaotozwa simu za mkononi zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
Mapendekezo hayo ni sehemu ya juhudi za serikali za kupunguza gharama kwa wananchi na kuimarisha uwezo wao wa kifedha.
Rais Ruto alitoa ahadi hiyo kwa mara ya kwanza jijini Eldoret Oktoba 20, 2026 wakati wa sherehe za siku kuu ya Mashujaa.
Hata hivyo pendekezo hilo ni lazima liidhinishwe kupitia bunge ambapo sheria zitafanyiwa marekebisho ili kupunguzia wakenya wa mapato ya chini mzigo wa ushuru ili wamudu gharama ya maisha.