Mabingwa mara nne wa Dunia Ujermani wataanza harakati za kuwania Kombe la Dunia, Jumapili usiku katika uwanja wa Houston, katika mechi ya kufungua kundi E dhidi ya Limbukeni Curacao.
Mechi hii ni sawia na vita vya Biblia baina ya Daudi na Goliathi,kisiwa hicho cha kutoka eneo la Concacaf, ikiwa taifa dogo zaidi kuwahikucheza Kombe la Dunia.
Curacao in idadi ya watu 150,000 na ukubwa wa ardhi ya maili 171 mraba.
Kocha wa Curacao Dick Advocaat anatarajiwa kuwajumuisha kaka wawili Juninho na Leandro Bacuna, ambao wakianza mechi ya Jumapili watajiunga na Jack na Bobby Charlton, pamoja na Yaya na Kolo Toure, kama ndugu waliocheza pamoja katika Kombe la Dunia.

Upande wake kocha wa Ujerumani Julian Nagelsman ,amedokeza kumwanzisha kipa mzoevu Manuel Neuer .
Ujerumani wanawinda Kombe la kwanza tangu mwaka 2014 nchini Brazil.