Kipute cha Kombe la dunia kitaingia siku ya tatu kati ya Jumamosi na Jumapili katika mataifa ya Marekani,Canada na Mexico.
Uswizi watakabiliana na waandalizi wa fainali za mwaka 2022 Qatar, katika uwanja wa San Francisco nchini Marekani katika kundi B kuanzia saa nne usiku.
Katika kundi C mabingwa mara tano Brazil watakuwa mjini Newyork, dhidi ya Morocco, saa saba usiku wa manane kabla ya Haiti, kukabiliana na Scotland saa kumi kesho alfajiri.
Australia itamenyana na Uturuki saa moja asubuhi kesho katika kundi D.
Mabingwa mara nne Ujerumani watacheza na limbukeni Curacao, katika kundi E, mjini Houston,Texas kisha Uholanzi, wamalize udhia na Japan.