Rais wa Shirikisho la kandanda nchini Kenya (FKF)Hussein Mohammed, alihudhuria kongamano la shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) mjini Miami nchini Marekani.
Kinara huyo ambaye anahudhuria fainali za Kombe la Dunia katika mataifa ya Mexico,Canada na Marekani, alikutana na Rais wa FIFA Gianni Infantino, wakati wa kongamano hilo.
Viongozi wa mshirikisho ya kandanda wanachama wa FIFA kote duniani walihudhuria kongamano hilo kupewa taarifa kuhusu maenndeleo na mikakati ijayo.
Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa katika kongamano hilo ni mwelekeo wa mradi wa FIFA Forward 4, na ufadhili wake,huku ukitarajiwa kuanza rasmi Januari mwaka ujao.

Aidha, wanachama walizungumzia kuhusu U15 World Cup Festival, unaongazia makuzi ya soka ya chipukizi na mipango ya kibiashara na ushirikiano.
Mohammed aliandamana na Kaimu Katibu Mkuu Dennis Gacheru kwenye kongamano hilo.
Ushiriki wa FKF katika kongamano hilo unaliainisha na FIFA.\, kuhusu ajenda ya maendeleo na kutumia kikamilifu fursa ibuka za kukuza soka kwa chipukizi.