Rais wa Cape Verde José Maria awazuru wachezaji baada ya kuwashika mateka Uhispania

Kiongozi kuyo alimsalimu na kumpongeza kila mchezaji na maafisa wote wa timu hiyo akisema ni fahari kubwa kwao kama taifa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Cape Verde President José Maria Neves, amewapongeza wachezaji na maafisa wa benchi ya kiufundi wa timu ya taifa maarufu kama blue Sharks, baada ya kulazimisha sare tasa dhidi ya Uhispania katika mechi ya Kombe la Dunia Jumatatu jioni.

Rais Neves alizuru chumba cha kubadilisha mavazi cha Cape Verde, punde baada ya mchuano huo na kuwapa heko wachezaji kwa matokeo hayo ya kihistoria.

Kiongozi kuyo alimsalimu na kumpongeza kila mchezaji na maafisa wote wa timu hiyo akisema ni fahari kubwa kwao kama taifa.

Kipa wa Blue Sharks Vozinha alitangazwa mchezaji bora wa mechi hiyo baada ya kupangua jumla ya mikwaju saba ya Uhispania.

Cape Verde ambao wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza watachuana na Uruguay na Saudi Arabia, katika mechi zilizosalia za kundi H.

Share This Article