Haji Manara ateuliwa Msemaji wa timu za soka Tanzania

Waziri Makonda amesema uteuzi wa Manara utaongeza upatishaji habari za timu zote za soka hadi kwa wananchi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,nchini Tanzanaia, Paul Makonda amemteua Haji Manara, kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za Tanzania za mchezo wa Soka.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Waziri Makonda amesema Haji atafanya kazi chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na atazisemea timu zote za Taifa za mpira wa miguu.

Manara amekuwa Msemaji wa vilabu vya Simba na Yanga kabla ya uteuzi wake.

Waziri Makonda amesema uteuzi wa Manara utaongeza upitishaji habari za timu zote za soka hadi kwa wananchi.

Share This Article