Chama soka nchini Ghana kimemteua Mreno Carlos Queiroz, kuwa kocha wa timu ya taifa Black Stars.
Queiroz ataiongoza Ghana kwa fainali za Kombe la Dunia mwezi Juni na Julai mwaka huu.
Mreno huyo anatwaa ukufunzi wa Black Stars kutoka Kwa Otto Addo aliyetimuliwa.
Queiroz mwenye umri Wa miaka 73, anaanza kampeini ya Ghana katika Kombe la Dunia Juni 17 dhidi ya Panama, kabla ya kukabiliana Na Uingereza na Croatia.
Queiroz amezinoa timu za Ureno, Iran,Misri, Oman, Japan na Qatar na pia vilabu vya Real Madrid na Manchester United.