Treni ya mizigo yarejelea safari za Athi River-Nyahururu baada ya miaka 46

Aidha, usafiri wa treni kati ya Athi River na Nyahururu utapunguza gaharama ya usafiri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Treni ya mizigo ya Shirika la Reli nchini lilisafirisha mizigo kutoka kituo cha Athi River kupitia Gilgil-Nyahururu kwa mara ya kwanza, ikiwa ni miaka 46 tangu safari za treni hiyo ya mizigo kusitishwa.

Katika safari hiyo ya kwanza, treni ilisafirisha tani 396 za mbolea ya serikali iliyopunguzwa bei kutoka kwa ghala ya Halmashauri ya Nafaka na Mazao (NCPB ) katika kituo cha Athi River hadi Nyahururu.

Mbolea hiyo itatumika na wakulima wa Nyahururu na Laikipia.

Treni hiyo inatarajiwa kufungua fursa nyingi za kibiashara kati ya Nyahuru na Athi River.

Aidha, usafiri wa treni kati ya Athi River na Nyahururu utapunguza gaharama ya usafiri.

Share This Article