Timu ya Uingereza yaibiwa viatu na mipira

Uingereza wataanza mazoezi mjini Kansas siku ya Jumapili kujiandaa kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Croatia wiki ijayo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Uingereza iliibiwa viatu na mipira vya ufanyia mazoezi Ijumaa usiku  kabla ya kuwasili katika kambi ya mazoezi ya Kansas nchini Marekani.

Chama cha soka nchini Uingereza kinajaribu kubaini vitu halisi vilivyoibwa huku ikishukiwa kuwa mipira na viatu ni miongoni mwa bidhaa zilizoibwa .

Yamkini wezi hao walivunja na kuingia kwenye kambi hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na kuwekwa vifaa hivyo kabla ya kuwasili kwa kikosi cha Uingereza.

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kufuatia kisa hicho, huku wakifanya msako wa wezi hao huku wezi  wawili wakiwa tayari wamenaswa.

Uingereza wataanza mazoezi mjini Kansas siku ya Jumapili, kujiandaa kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Croatia wiki ijayo.

Share This Article