Samba Boys wahemeshwa na Simba wa Atlas

Hadi kipenga cha mwisho Morocco waliomaliza wa nne miaka minne iliyopita nchini Qatar, walipata alama moja muhimu dhidi ya Selecao ya Brazil.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara tano wa Dunia Brazil almaarufu Samba Boys, walilazimishwa kutoka nyuma ili kupata sare ya bao moja dhidi ya timu bora barani Afrika Morocco, ukipenda Atlas Lions.

Mechi hiyo ya ufunguzi kundini C ilisakatwa usiku wa manane Jumamosi,katika uchanjaa Metlife, huku Morocco wakianza  vyema dakika 15 za kwanza kwa pasi za kuonana na kuwalazimu Brazil kujihami dhidi ya kufungwa bao mapema.

Hata hivyo ,Brazil walitulia mchezoni kuanzia robo saa ya mchezo .

Kunako dakika ya 21 Morocco walipiga shambulizi la kushtukiza Brahim Diaz, akimpakulia pasi murua Ismael Saibari  ambaye bila kusita alipachika bao la ufunguzi.

Samba Boys wa walirejea mchezoni kunako dakika ya 32  kupitia kwa Vinicius Junior, aliyeunganisha pasi ya Bruno Guimares.

Kutoka hapo pande zote zilicheza kwa tahadhari makipa wote Yassin Bonou na Allison Becker, wakiwa na kazi ya ziada kupangua matobwe.

Hadi kipenga cha mwisho Morocco waliomaliza wa nne miaka minne iliyopita nchini Qatar, walipata alama moja muhimu dhidi ya Selecao ya Brazil.

Share This Article