Qatar yalazimisha sare ,Scotland washinda

Uswizi walikuwa wa kwanza kupachuika bao kupitia kwa penati ya Breel Embolo kunako dakika ya 17, kabla ya Miro Muheoim kujifunga kunako dakika ya 94.

Dismas Otuke
1 Min Read

Qatar walipata pointi moja ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia,walipotoka sare ya bao moja dhidi ya Uswizi katika mechi ya kundi B,mechi  iliyopigwa Jumamosi usiku mjini San Francisco nchini Marekani.

Uswizi walikuwa wa kwanza kupachuika bao kupitia kwa penati ya Breel Embolo, kunako dakika ya 17, kabla ya Miro Muheoim kujifunga kunako dakika ya 94.

Katika kundi C Scotland wanaoshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza walisajili ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Haiti, uwanjani Gillette nchini Marekani mapema Jumapili.

John McGinn alitikisa wavu katika kipindi cha kwanza na kuwapa Scotland, ushindi ambao umewachupisha kileleni pa kundi C kwa alama 3,wakifuatwa na Brazil na Morocco kwa pointi moja kila moja.

Share This Article