FIFA World Cup:Australia yaigutusha Uturuki

Matokeo hayo yana maana kuwa Australia wanaongoza kundi D pamoja na Marekani kwa alama 3 kila moja.

Dismas Otuke
0 Min Read

Australia waliwagutusha Uturuki baada ya kuwacharaza mabao 2-0, katika mechi ya Kundi D, iliyoandaliwa Jumapili asubuhi mjini Vancouver,Canada.

Mzawa wa Burundi,Nestory Irankunda na Connor Metcalfe ,walipachika bao moja katika kila kipindi huku Socceroos, wakiepuka kushinda mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia.

Matokeo hayo yana maana kuwa Australia wanaongoza kundi D pamoja na Marekani kwa alama 3 kila moja.

Share This Article