Timu ya taifa ya Kenya ,Harambee Stars,itachuana na Lesotho katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki mwezi ujao.
Kulingana na shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) mechi mbili za awali dhidi ya Palestine na Kyrgyzstan, zimefutiliwa mbali kutokana na changamoto za ufasiri.
Harambee Stars watacheza dhidi ya Lesotho katika mechi ya kwanza Juni 4 na ya pili Juni 7, katika uwanja wa Lucas Moripe mjini Pretoria,Afrika Kusini.
Kenya itafungua mechi za kundi D kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao dhidi ya Eritrea, Septemba 21 jijini Nairobi, kabla ya kuizuru Guinea Oktoba 6.
Kikosi cha Harambee Stars kwa mechi hizo mbili za kirafiki kinawajumuisha:
Makipa: Byrne Omondi, Faruk Shikhalo, Caleb Kramer.
Mabeki: Erick Ouma, Stanley Wilson, Sylvester Owino, Frank Odhiambo, Alphonce Omija, Deon Woodman, Rooney Onyango, Sydney Agina.
viungo: Richard Odada, Chris Erambo, Clarke Odour, Will Lenkupae, Austine Odhiambo, Zech Obiero.
Washambulizi: Job Ochieng, Mohammed Bajaber, Ben Stanley, Sammy Hena-Kamau, Micah Obiero, Ryan Ogam, Lawrence Okoth.