Misri, Ivory Coast, Tunisia na Cape Verde kushuka uwanjani Jumatatu

Uhispania ambayo inaorodhoshwa ya pili bora duniani itamenyana na wawakilishi wa Afrika Cape Verde, wanaoshiriki kwa mara ya kwanza  katika kundi H.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wawakilishi wanne wa Afrika watashuka uwanjani kuanzia usiku wa manane Jumatatu, kwa mechi za ufunguzi za Kombe la Dunia linaloendelea.

Tembo wa Ivory Coast wanaorejea kwenye kipute hicho baada ya miaka 12, wataanza harakati zao kundini E dhidi ya Ecuador ya Amerika Kusini.

Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Philadelphia.

Ivory Coast watalenga kuondoa nuksi ya kupoteza kila mechi  ya Kombe la Dunia wanapocheza na wapinzani wa kutokea Marekani Kusini.

Baadaye, saa kumi na moja alfajiri, itakuwa zamu ya The Carthage Eagles ya Tunisia kukabiliana na Uswidi uwanjani Monterrey nchini Mexico.

Tunisia wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mtawalia.

Uhispania ambayo inaorodhoshwa ya pili bora duniani itamenyana na wawakilishi wa Afrika Cape Verde, wanaoshiriki kwa mara ya kwanza katika kundi H.

Mchuano huo utachezwa katika uwanja wa Mercedes Benz kuanzia saa moja usiku.

Hatimaye, saa nne usiku, Ubelgiji na Misri watakutana kwa mara ya kwanza katika historia katika mechi ya kundi G nchini Marekani.

 

 

 

Share This Article