Kenya na Afrika Kusini zatia saini Mikataba 6 ya Kibiashara

Mikataba hiyo inajumuisha uchukuzi na uchumi wa baharini, usawa wa kijinsia na uwezeshaji, mafunzo ya kiufundi, sanaa, utamaduni, turathi na michezo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William ruto na mwenzake wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa washuhudia kutiwa saini kwa Mikataba sita ya Kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Kenya na Afrika Kusini zimetia saini Mikataba sita ya kibiashara, hii ikitajwa ishara ya kujitolea kwa nchi hizo mbili kuimarisha ushirikiano kati yao.

Rais William Ruto na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini walishuhudia hafla hiyo iliyoandaliwa katika jumba la Union Jijini Pretoria.

Mikataba hiyo inajumuisha uchukuzi na uchumi wa baharini, usawa wa kijinsia na uwezeshaji, mafunzo ya kiufundi, sanaa,utamaduni,  turathi na michezo.

Kupitia ukurasa wa X, Rais Ruto alisema mikataba hiyo inalenga kuinua ushirikiano, uliojikita kwenye msingi thabiti ambao umekuzwa kwa muda wa miongo mitatu.

Rais William Ruto yuko katika ziara ya siku mbili nchini Afrika Kusini, akilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya Kenya na Afrika Kusini kupitia misururu ya mazungumzo yatakayolenga upanuzi wa biashara na uwekezaji, ujumuishaji wa kikanda, ushirikiano wa amani na usalama na kupanua maendeleo kote barani.

Share This Article