Watu 773 wameuawa mjini Goma wiki moja iliyopita

Dismas Otuke
1 Min Read

Watu wapatao 773 wameuawa katika mji wa Goma, ambao ni mji mkubwa zaidi ulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ndani ya siku saba zilizopita.

Watu hao waliuawa kufuatia makabiliano makali baina ya waasi wa M23 ambao wametewaa maeneo mengi ya mji huo na wanajeshi wa serikali.

Hata hivyo, huenda idadi hiyo ikawa kubwa zaidi kwani waasi waliwaamrisha raia kusafisha barabara na kuondoa miili iliyozagaa mjini Goma.

Msemaji wa serikali ya DRC Patrick Muyaya aliwaarifu wanahabari jana Jumapili kuwa huenda kuna miili iliyozikwa katika makaburi ya pamoja.

Wakati huo huo, mamia ya wakazi wa Goma walianza kurejelea shughuli za kawaida mjini humo juzi Jumamosi baada ya waasi wa M23 kuahidi kurejesha huduma muhimu zilizokatizwa kama maji na umeme.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *