Watu kadhaa walijeruhiwa baada ya basi la abiria lijulikanalo kama Nganya kubingiria katika barabara ya Enterprise eneo la Viwandani jana Jumatano usiku.
Yamkini basi hilo lilikuwa katika mwendo wa kasi huku likiendeshwa kiholela, kabla ya dereva kupoteza mwelekeo na basi kuanguka na kisha kubingiria.
Wengi wa waliojeruhiwa ni wale waliokuwa wamedandia mlangoni baada ya kudondoka na kuangukiwa na basi hilo.
Kulingana na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu waliofika eneo la ajali, watu kadhaa walipokea huduma ya kwanza na wengine kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.