Waziri wa Elimu Julis Migos Ogamba amefunga shule ya upili ya Utumishi Girls Academy mara moja kufuatia mkasa wa moto uliotokea usiku wa manane siku ya Alhamisi.
Moto huo ulisababisha vifo vya wanafunzi 16 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Akizungumza alipozuru shuleni humo kutathmini athari za mkasa huo, Waziri Ogamba amesema ameifunga shule hiyo ili kuruhusu uchunguzi kufanywa kuhusu chanzo chake.
Ogamba amefichua kuwa moto huo ulizuka saa saba kasorobo usiku huku wanafunzi 71 waliokumbwa na majeraha wakitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 200 wakati wa mkasa huo, huku 16 wakiangamia baada ya kushindwa kutoroka.
Waziri ameziliwaza familia za waathiriwa akiahidi uchunguzi wa kina kubaini ikiwa mikakati yote ya kiusalama ilikuwa imewekwa shuleni humo.