Wizara ya Elimu imetoa shilingi bilioni 19 ikiwa sehemu ya shilingi bilioni 33 za kufadhili masomo kwa muhula wa kwanza mwaka huu.
Waziri wa Elimu Julius Ogambo kwenye mahojiano ya kipekee kupitia runinga ya KBC Channel 1, amesema kwamba baada ya kutoa shilingi bilioni 19, wameanza mchakato wa kusambaza shilingi bilioni 14 ili kufanya kiasi cha fedha zilizotengewa muhula wa kwanza kufikia shilingi bilioni 33 .
Aidha, Ogamba amefafanua kuwa kutokana na changamoto za kiuchumi, serikali haingeweza kutoa shilingi bilioni 49 zilizohitajika kugharimia masomo muhula huu wa kwanza.
Kuhusu matokeo ya hivi majuzi ya kidato cha nne KCSE, Waziri amesema kuwa wanafunzi 260,000 walipata alama za kujiunga na vyuo vikuu.
Kwa mara ya kwanza pia, Wizara ya Elimu imeanzisha mtihani wa katikati ya mwaka kwa wanafunzi wanaotaka kuboresha matokeo yao ili kujiunga na vyuo vikuu mwezi Septemba mwaka huu.