Papa Leo XIV amemteua Kasisi John Mwandi kuwa kuongoza dayosisi ya Kitui ya kanisa Katoliki.
Hadi uteuzi wake, Kasisi Mwandi alikuwa Naibu wa Kasisi Joseph Mwongela, ambaye amehamishwia Dayosisi ya Machakos.
Kasisi Mwongela anatarajiwa kuchukua mahali pa Kasisi wa sasa Norman King’oo ambaye muda wake wa kustaafu unakaribia.
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican, yalitangaza uteuzi wa Kasisi Mwandi katika hatua ambayo imepongezwa na waumini wa kanisa na viongozi wa kidini katika eneo hilo.
Akizungumza baada ya uteuzi wake, Kasisi Mwandi alielezea furaha yake huku akiahidi kuimarisha dayosisi hiyo na kupigia debe umoja miongoni mwa jamii ya waumini Wakatoliki.