Polisi akamatwa juu ya mauaji ya wakili Mathew Kyalo Mbobu

Kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea, makachero wamepata bastola aina ya Ceska ambayo mshukiwa alipatiwa wakati wa tukio hilo.

Martin Mwanje
1 Min Read
Marehemu wakili Mathew Kyalo Mbobu

Wapelelezi wamemkamata Konstebo wa Polisi Julius Cheruiyot kuhusiana na mauaji ya wakili Mathew Kyalo Mbobu mwaka mmoja uliopita. 

Mbobu alifyatuliwa risasi na kuuawa Septemba 9, 2025 kwenye barabara ya Magadi wakati akielekea nyumbani mtaani Karen.

Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI inasema baada ya upelelezi wa kukuna kichwa uliofanywa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, imemtambua na kumkamata Cheruiyot kwa tuhuma za kufyatua risasi na kumuua wakili huyo.

“Kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea, makachero leo walipata bastola aina ya Ceska ambayo mshukiwa alipatiwa wakati wa tukio hilo, ilisema DCI kupitia msemaji wake John Marete.

“Uchunguzi wa kibalistiki umebaini kuwa hakika silaha hiyo ilitumika katika ufyatuaji risasi uliomuua wakili Mbobu. Matokeo yanatoa mafanikio makubwa ya kisayansi katika uchunguzi huo na kuimarisha zaidi ushahidi unaokusanywa na makachero.”

Kadhalika, DCI inasema uchunguzi wao umebaini kuwa Inspekta Kenneth Sang, ambaye kwa sasa ameenda mafichoni, anadaiwa kuratibu operesheni hiyo kwa kushirikiana na mwanasiasa Rose Mbithe ambaye kwa sasa yuko korokoroni.

Mbithe anazuiliwa na wanawe wawili kuhusiana na mauaji ya Dkt. Victoria Mutiso.

 

Share This Article