Tusker FC ya Kenya itawaalika Al Ahli Madanii FC kutoka Sudan, katika marudio ya mchujo wa kwanza kuwania kombe la shirikisho Afrika, katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo kuanzia saa tisa alasiri.
Wagema Mvinyo Tusker waliotoka sare ya 2-2 wiki jana katika duru ya kwanza mjini Kigali,Rwanda,wanahitaji sare tasa ili kufuzu kwa mchujo wa pili ambapo watacheza dhidi ya singida Black Stars ya Tanzania.
Tusker wanarejea katika Kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2021/2022, walipobanduliwa na miamba wa Misri,Zamalek katika mchujo wa pili.
Singida kwa upande wao wamefuzu kwa mchujo wa pili baada ya kuwakomoa Al Ghazal ya Sudan Kusini mabao 7-1, na watakuwa nyumbani leo kukamilisha ushindi huo mkubwa.
Timu 16 zitakazoshinda mchujo wa pili zitafuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe hilo.