Kenya, Rwanda, Misri na Cameroon wafuzu robo fainali ya Voliboli kwa wanawake Afrika

Malkia Strikers waliokuwa wamewashinda Zambia seti 3-0 katika mechi ya ufunguzi wanaongoza kundi hilo kwa alama sita huku Senegal ikiwa na alama 3 wakati Burkina Faso ikiburura mkia bila alama.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Kenya, Misri, Rwanda na Cameroon walifuzu kwa robo fainali ya mashindano ya Voliboli Afrika kwa wanawake yanayoendelea baada ya kushinda mechi zote tatu za makundi yao.

Malkia Strikers wa Kenya walijihakikishia nafasi ya kwanza kundini A baada ya kuwashinda Mali seti 3-0 za 25-17, 25-10, na 25-18 katika mchuano wa pili Alhamisi usiku katika uwanja wa Kasarani.

Malkia Strikers waliokuwa wamewashinda Zambia seti 3-0 katika mechi ya ufunguzi wanaongoza kundi hilo kwa alama sita huku Senegal ikiwa na alama 3 wakati Burkina Faso ikiburura mkia bila alama.

Cameroon wako kileleni pa kundi C kwa alama 9 wakifuatwa na Tunisia kwa pointi 4, huku Ghana na Nigeria wakifuatana kwa alama 3 na 2 mtawalia.

Rwanda waliongoza kundi D kwa pointi 9 kufuatia ushindi wa mechi tatu wakifuatwa na Algeria kwa alama 6 wakati DRC wakiwa na alama 3.

Share This Article