Aliyekuwa Gavana wa jimbo la Nairobi,Mike Sonko aliituza timu ya wanawake ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17, shilingi milioni moja pesa taslimu baada ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Sonko aliwasilisha kitita hicho kwa timu hiyo katika chumba cha kubadilisha mavazi punde baada ya mechiya Jumapili.
Kenya ilijikatia tiketi baada ya kuishinda Afrika Kusini mabao 3-1, katika mechi ya marudio Jumapili jioni katika uwanja wa Nyayo, huku ikifuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1.
Sonko alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa uwanjani Nyayo, kuitazama mechi ya Junior Starlets dhidi ya Bantwana ya Afrika Kusini.
Kenya itashiriki Kombe la Dunia nchini Morocco kati ya Oktoba 17 na Novemba 7 mwaka huu .
Junior Starlets wamejumuishwa kundi E,pamoja na Marekani,Samoa na Uchina katika fainali hizo za Kombe la Dunia.