Rais William Ruto akariri kuboresha miundo mbinu ya michezo

Aidha, Ruto alisema kuwa serikali inalenga kujenga uwanja katika kila eneo kati ya maeneo manane nchini na pia academia 37 za michezo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto, amekariri kujitolea kwa serikali kuboresha miundo mbinu ya michezo nchini ili kukuza vipaji.

Rais amesema haya mapema Jumanne alipoandaa staftahi kwa wachezaji wa klabu za Police FC na Police Bullets FC, zilizotwaa ubingwa wa ligi kuu za soka msimu huu.

Aidha, Ruto alisema kuwa serikali inalenga kujenga uwanja katika kila eneo kati ya maeneo manane nchini na pia academia 37 za michezo.

Aliwataka wahisani kusaidia juhudi za ukuzaji michezo kutoka mashinani.

Website |  + posts
Share This Article