Mashindano ya kitaifa ya riadha na majarabio ya kitaifa yamepigwa jeki, baada ya benki ya Kenya Commercial-KCB, kutangaza ufadhili wa shilingi milioni 8.
Ufadhili huo utashuhudia shilingi milioni 4 ,zikigharamia mashindano ya kitaifa ya siku tatu kuanzia kesho hadi Ijumaa katika uwanja wa Ulinzi Complex na kiwango kingine sawia kwa majaribio ya kitaifa ya kuteua kikosi cha Kenya kwa mashindano ya Dunia kati ya Agosti 1 na 2.
Wanariadha kadhaa akiwemo bingwa wa dunia katika mita 800 Mary Moraa,bingwa Dunia katika mita 800 kwa chupukizi chini ya umri wa miaka 20 Sarah Moraa, na mabingwa wa kitaifa katika mita 400 kuruka vizuizi na mita 400 Wiseman Were na Bonifacce Mweresa wamesema wako tayari kwa mashindano hayo .
Mashindano ya kitaifa yataandaliwa kati ya kesho na Ijumaa katika uwanja wa Ulinzi Complex, huku yakiwashirikisha wanariadha kutoka maeneo yote 12 ya chama cha riadha Kenya AK na wale wa kutoka KDF,Prisons,Police na vyuo vikuu watashiriki.