Diego Forlan ateuliwa Kocha Mkuu wa Uruguay

Shirikisho la soka nchini Uruguay (AUF) limemtangaza Forlan kama kaimu kocha kutwaa nafasi iliyoachwa kufuatia kung'atuka kwa Marcelo Bielsa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa zamani wa Atletico Madrid, Diego Forlan, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uruguay hadi Machi mwaka 2027.

Shirikisho la soka nchini Uruguay (AUF) limemtangaza Forlan kama kaimu kocha kutwaa nafasi iliyoachwa kufuatia kung’atuka kwa Marcelo Bielsa.

AUF, imesema kuwa itathmini mkaba wa mwanandinga huyo wa zamani wa timu ya taifa baada ya mkataba wake kukamilika mwaka ujao.

Forlan aliye na umri wa miaka 47, ataiongoza Uruguay, kwa mechi za kirafiki kuanzia Septemba mwaka huu na Machi mwaka ujao.

Hadi uteuzi wake forlan amekuwa kocha wa klabu ya Penarol mwaka 2011, na klabu ya Atenas de San Carlos mwaka 2021.

Share This Article