Ruto ahimiza ushiriakiano kati ya Kenya na Afrika Kusini ili kufungua fursa

Aliongeza kuwa licha ya kuwa ushirikiano wa kibiashara baina ya nchini hizi mbili upo, mengi yapaswa kufanywa ili kuwezesha ufanisi zaidi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amehimiza haja ya kuboresha ushirikiano kati ya Kenya na Afrika Kusini, ili kupanua fursa za kimaendeleo kwa raia wa mataifa hayo mawili.

Aliongeza kuwa licha ya kuwa ushirikiano wa kibiashara baina ya nchini hizi mbili upo, mengi yanapaswa kufanywa ili kuwezesha ufanisi zaidi.

Rais Ruto alitetea mikataba ambayo Kenya ilisaini na Afrika Kusini katika ziara yake akisema itarahishisha biashara, kuimarisha utangamano wa kikanda na kuboresha miundombinu miongoni mwa mafao mengine.

Ruto aliyasema hayo Alhamisi usiku alipohutubia kikao cha wawekezaji na wafanyabiashara wa Kenya na wale wa Afrika Kusini mjini Jonannesburg.

Ruto aliandamana na mwenyeji wake Cyril Ramaphosa katika kikao hicho.

Share This Article