Katibu wa Wizara ya Leba Shadrack Mwadime amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Muungano wa ujuzi na maarifa barani Afrika (SASANET).
Mwadime alichaguliwa wakati wa mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka wa SASANET, ulioandaliwa mjini Abuja,Nigeria tarehe 3 mwezi huu.
Wajumbe waliohudhuria kikao hicho kwa kauli moja walimchagua Mwadime ambaye sasa anajukumiwa kuongoza ushirikiano wa kitaaluma na ujuzi Afrika, kwa kuainisha na shirika la kimataifa la wafayakazi (ILO) kipengee cha 208 kinachopendekeza kuwa na mfumo wa kutuoa mafunzo ya ujuzi na taaluma unaowajumuisha wote na kuwepo kwa mazingira bora ya kufanyia kazi.
Ujumbe wa Kenya katika kikao hicho cha Abuja uliwajumuisha Katibu wa ukuzaji maarifa Wanjiru Kariuki, na Afisa Mkuu mtendaji wa Shirikisho la vyama vya Jua Kali Associations (KNFJKA) Wambua Nyamai.