Shule ya Upili ya St.George’s yafungwa kwa muda

Kwenye barua iliyoandikwa na usimamizi wazazi walishaurikiwa kufika shuleni mapema Ijumaa kuwachukua wanafunzi wao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shule ya Sekondari ya wasichana ya St. Georges iliyo kaunti ya Nairobi,imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya mtafaruku kuzuka miongoni mwa wanafunzi.

Kwenye barua iliyoandikwa na usimamizi wazazi walishaurikiwa kufika shuleni mapema Ijumaa kuwachukua wanafunzi wao.

Inafahamika kuwa wanafunzi walitishia kuzua vurugu baada ya kutolewana na walimu ndiposa usimamizi wa shule ukahiari kuwaruhusu kwenda nyumbani.

Kisa hicho ni cha hivi punde huku zaidi ya shue tano zikifunga na kuwaachilia wanafunzi kwenda nyumbani tangu wiki jana.

Share This Article