Mechi za mwisho za makundi za mchezo wa soka kwa wavulana na wasichana kwenye makala ya 23 ya mashindano ya shule za upili Afrika mashariki zitapigwa Jumanne mjini Morogoro,Tanzania.
Katika mechi za soka ya wavulana kundini A ,Iptem Makamba ya Burundi itamenyana na wenyeji Mbeya huku Nzumba ya Tanzania ikipimana nguvu na Amusi College ya Uganda.
Kundini B,St Mary’s Yala ya Kenya itakabiliana na CGF Kigali ya Rwanda nao St Mary’s Kitende kutoka Uganda wamalieze udhia na Morogoro ya Tanzania.
Kakamega ya Kenya itakuwa na miadi dhidi ya Bukedea ya Uganda,wakiilishi wa Kenya wakihitaji ushindi ili kuwa matumaini ya kuingia mwondoano nayo Kyandondo ihitimishe ratiba dhidi ya Urambo ya
Tanzania katika kundi C.

Katika soka ya wasichana Jinja Preogressive ya Uganda itamenyana na wenzao Rines katika kundi A wakati Fountain Gate kutoka Tanzania wakishuka uwanjani dhidi ya Ziba pia ya Tanzania.
PSB Huye kutoka Rwanda itashikana mashati na Nyakach Girls ya Kenya katika mchuano mwingine wa kundi A.

Katika kundi B,St Joseph Girls ya Kitale itapambana na Boni Consil Girls ya Uganda huku Kilombero na Alliance Secondary zote za Tanzania zikimaliza udhia katika kundi B.