Mabingwa watetezi Nigeria, almaarufu Super Falcons, wanashiriki fainali za Kombe bara Afrika-WAFCON zinazoanza leo Jumapili usiku nchini Morocco wakiwinda Kombe la 11.
Nigeria wamenyakua mataji kumi miaka ya 1998, 2000, 2002, 2004, 2006, 2010, 2014, 2016, 2018 na 2024.
Super Falcons watafuangua uetezi wa Kombe hilo Jumanne hii Julai 28, dhidi ya Malawi katika kundi C,kabla ya kupambana na Zambia,Agosti Mosi na hatimaye Misri siku nne baadaye.
Equitorial Guinea wametawazwa mabingwa mara mbili 2008 na 2012 wakati Afrika Kusini, ikishinda Kombe hilo mwaka 2022.
Algeria watafungua kipute hicho dhidi ya Senegal saa mbili usiku Jumapili baada ya sherehe za ufunguzi, kabla ya kuwapisha wenyeji Morocco, dhidi ya Kenya, saa tano usiku.
Makundi ya WAFCON 2026
Kundi A – Rabat: Morocco, Algeria, Senegal, Kenya
Kundi B – Casablanca: South Africa, Côte d’Ivoire, Burkina Faso, Tanzania
Kundi C – Rabat: Nigeria, Zambia, Egypt, Malawi
Kundi D – Casablanca: Ghana, Cameroon, Mali, Cape Verde