Kenya yawinda alama ya kwanza WAFCON

Kenya ilipoteza mechi zote tatu ilizocheza mwaka 2016, wakifunga mabao 2 .

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya wanawake ya Kenya itakabiliana na Morocc katika  mechi ya pili kundini A kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika – WAFCON,Jumapili usiku katika uchanjaa wa Moulay El Hassan jijini Rabat nchini Morocco.

Kenya itacheza mechi hiyo ikisaka ushindi au sare ya kwanza katika historia ya Kombe hilo baada ya kupoteza mechi zote tatu iliposhiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2016.

Kenya ilipoteza mechi zote tatu ilizocheza mwaka 2016, wakifunga mabao 2 .

Timu nyingine kundini A na Kenya ni Algeria na Senegal.

Fainali hizo za WAFCON ambazo ziliahirishwa kutoka mwezi Aprili mwaka huu zitatumika kubaini timu tatu zitakazocheza  Kombe la Dunia mwaka ujao.

Itakuwa mara ya kwanza kwa kipute cha WAFCON kushirikisha timu 16 baada ya kuongezwa kutoka 12 za awali.

 

 

Share This Article